Maelezo ya chama cha kikomunist

 

UTANGULIZI KWA MCHAPO WA KIJERUMANI WA MWAKA 1890

 

F. Engels

 


Tarehe ya kuandika: Katika mai 1890, kwa Friedrich Engels.
Tarehe ya kuchapishwa: Katika 1890.
Toleo hili: Marxists Internet Archive (marxists.org),februari 2013.
Chanzo cha Nakala: Karl Marks na Frederick Engels, Maelezo y Chama cha Kikomunist, Moscow, Idara ya Maendeleo (1965).


 

 

Tangu huo hapo juu ulipoandikwa,[1] mchapo mpya wa Kijerumani wa "Maelezo" umekuwa tena unahitajiwa, na pia mengi yametokea kwa "Maelezo" hayo yenyewe ambayo lazima yaandikwe hapa.

Tafsiri ya pili ya Kirusi - iliyofanywa na Vera Zasulich[2] - ilitokeza Geneva katika mwaka 1882; utangulizi kwa tafsiri hiyo uliandikwa na Marks na mimi. Kwa bahati mbaya, maandishi уa asili kwa Kijerumani yamepotea; kwa hivyo imenibidi niifasiri kinyume kutoka katika lugha ya Kirusi, ambayo kwa njia yo, yote haitayatengeneza mambo yaliyomo[3] Nayo ni kama hivi:

"Mchapo wa mwanzo wa Kirusi wa 'Maelezo ya Chama cha Kikomunist,' uliofasiriwa na Bakunin, ulitokea mapema katika miaka ya sitini ya karne ya 19 katika nyumba у a kuchapia vitabu уa Kolokol[4] Wakati huo watu wa Magharibi waliweza kuuchukulia mchapo wa Kirusi wa 'Maelezo' kama ni maandishi ya kuchekesha tu. Maoni kama hayo yasingewezekana kuwapo leo.

"Jinsi nyendo za wafanya kazi zilivyokuwa zimeshikilia mahali padogo tu wakati huo (Desemba 1847) inaonyeshwa wazi wazi na sehemu ya mwisho ya 'Maelezo' hayo: 'Msimamo wa wakomunist kuhusu vyama mbalimbali vya upinzani katika nchi mbalimbali/ Hasa Urusi na Marekani hazipo hapo. Ulikuwa ni wakati ambapo Urusi ilikuwa ndiyo mlimbiko mkubwa wa mwisho wa nguvu za upingaji maendeleo wote wa Ulaya, ambapo wafanya kazi waliozidi katika Ulaya walikuwa wakihamia Marekani. Nchi zote mbili zilikuwa zikiipa Ulaya vitu visivyotengenezwa na pia zilikuwa ni masoko kwa kuuzia bidhaa za uchumi. Wakati huo nchi zote mbili kwa hivyo, kwa hali hii au nyingine, zikawa ndio nguzo kubwa za utaratibu ulioko Ulaya.

"Jinsi gani mambo yalivyo tofauti kabisa leo! Hasa kuhama Ulaya kulisaidia maendeleo makubwa sana ya ukulima katika Marekani, ambao ushindani wake unaitikisa misingi yenyewe hasa ya wenye kumiliki mashamba wa Ulaya - wakubwa na wadogo. Isitoshe, kumeiwezesha Marekani kuzitumilia nguvu zake nyingi sana za uchumi kwa nguvu na kwa wingi mkubwa ambao lazima baada ya muda mchache uivunjilie mbali hali у a kuhozi uchumi wote у a Ulaya у a Magharibi, na hasa ya Uingereza, iliyopo mpaka sasa. Hali zote mbili zitaleta athari ya kithawra kwa Marekani yenyewe. Kidogo kidogo wakulima wenye kumiliki vipande vidogo vya ardhi na vya kiasi, msingi wa utaratibu wake wa kisiasa, wanaanza kuanguka katika mashindano dhidi ya wenye mashamba makubwa; papo hapo, umma mkubwa wa wafanya kazi na mkusanyiko wa rasilmali nyingi sana unakua kwa mara ya mwanzo katika sehemu zenye uchumi.

"Na sasa Urusi! Wakati wa Thawra ya miaka 1848-1849 si wafalme wa Ulaya tu, lakini hata mabepari wa Ulaya pia, wameona kuwa hapana njia nyingine ya kuokoka kutokana na wafanya kazi, ambao ndio kwanza wanaanza kuamka, isipokuwa kutegemea msaada wa Urusi. Mfalme wa Urusi, alitangazwa kuwa ndiye mkuu wa wapingaji maendeleo wa Ulaya. Leo yeye ni mahabusi wa thawra, katika Gatchina, na Urusi imekuwa ndiyo kikundi cha mbele cha nyendo za kithawra katika Ulaya.

"Kazi ya 'Maelezo ya kikomunist' ilikuwa ni kutangaza ukomeshaji ulio karibu sana usioweza kuepukika wa miliki ya sasa ya kibepari. Lakini katika Urusi tunakuta, ikikabiliana uso kwa uso na maendeleo makubwa ya kikepitalist yanayokuwa mbio mbio na miliki ya kibepari ya ardhi ambayo ndiyo kwanza ianzishwe, zaidi kuliko nusu ya ardhi yote inamilikiwa na wakulima kwa mujibu wa utaratibu wa obshchina. Sasa swali lililoko ni kwamba: obshchina ya Kirusi, ingawa utaratibu huo wa kikale wa kumiliki ardhi kwa pamoja umepunguzwa sana umuhimu wake, unaweza kukiuka moja kwa moja kuingia utaratibu wa juu kabisa wa aina у a kumiliki ardhi, yaani ya kikomunist? Au kinyume cha hayo, lazima kwanza ipitie njia ile ile ya kuvunjika kama ilivyo katika mabadiliko ya kihistoria ya Magharibi? Jawabu moja tu inayowezekana kutolewa kwa leo ni hii: pindi thawra ya Urusi itakuwa ndiyo ishara kwa thawra ya wafanya kazi katika Magharibi, ili kwamba zote mbili ziwe zinasaidiana, basi hali ya sasa ya kumiliki ardhi kwa pamoja katika Urusi yaweza kutumika kama ndio chanzo cha maendeleo ya kikomunist.

Karl Marks. F. Engels

London, tarehe 21 Januari, 1882

Kiasi cha wakati huo huo, tafsiri mpya ya Kipolish ilitokeza katika Geneva: "Manifest Kommunistyczny".

Zaidi ya hayo, tafsiri mpya ya Kidenish imetoka katika Socialdemokratisk Bibliothek, Kjobenhavn 1885. Kwa bahati mbaya haikukamilia kabisa; baadhi ya sehemu muhimu, ambazo zinaonyesha zilimpatisha taabu mtu aliyefasiri, zimeachwa, na isitoshe pana dalili za kutokuwa na hadhari katika kufasiri mahali hapa na pale, ambazo inasikitisha hasa kuziona ilivyokuwa tafsiri hiyo inaonyesha kwamba laiti mtu aliyefasiri angalijitahidi zaidi kidogo angalikuwa amefanya kipande chema kabisa cha kazi.

Tafsiri mpya ya Kifaransa ilitokea mwaka 1886[5] katika gazeti la Paris Le Socialiste; ndiyo tafsiri bora kabisa iliyopata kuchapwa mpaka sasa.

Kutokana na hiyo ya pili tafsiri ya Kispanish ilichapwa mwaka huo huo, kwanza katika gazeti la Madrid El Socialista[6] na halafu ikatolewa tena kama kijitabu: Manitiesto del Partido Comunista, por Carlos Marx у F. Engels, Madrid, Administration de El Socialista, Hernan Cortes 8.

Kama ni jambo la kuchekesha ninaweza pia kutaja kwamba katika mwaka 1887 maandishi ya tafsiri ya Kiarmenia ya "Maelezo” yalitolewa kupewa mchapaji katika mji wa Constantinople. Lakini mtu huyo mwema hakuwa na moyo wa kuchapa kitu cho chote chenye jina la Marks na akatoa shauri kwamba mtu huyo aliyefasiri atoe jina lake mwenyewe kama ndiye mtungaji, lakini huyo wa pili, akakataa.

Baada ya kuchapwa tena kwa mfululizo katika Uingereza tafsiri mbalimbali za Kimarekani zilizokuwa kidogo si barabara, tafsiri halisi mwishowe ilitokea katika mwaka 1888. Hii ilikuwa imefanywa na rafiki yangu Samuel Moore, na tukaipitia sote pamoja kwa mara у a mwisho kabla haikupelekwa kwenda kuchapwa. Imeitwa: "Manifesto of the Communist Party, by Karl Marx and Frederick Engels. Authorized English Translation, edited and annotated by Frederick Engels. 1888. London, William Reeves, 185 Fleet st. E. C."[7] Baadhi ya maelezo ya mchapo huo yametiwa katika mchapo huu wa sasa.

"Maelezo" yamekuwa na taarikh yake yenyewe. Yakipokelewa kwa hamu sana, wakati wa kutokeza kwake, na viongozi wa usoshialist wa kisayansi ambao kwa wakati huo hawakuwa wengi (kama ihakikishwavyo na tafsiri zilizotajwa katika utangulizi wa mwanzo), mara yakasukumwa nyuma na upingaji wa maendeleo ulioanza baada ya kushindwa kwa wafanya kazi wa Paris katika Juni mwaka 1848, na mwishowe yakaharamishwa "kwa mujibu wa sheria" pamoja na kuhukumiwa kwa wakomunist wa Cologne katika Novemba mwaka 1852. Kwa upoteaji machoni pa watu wa nyendo za wafanya kazi zilizoanza pamoja na Thawra ya Februari, "Maelezo" pia yakafichika.

Wakati tabaka уa wafanya kazi wa Ulaya ilipckwisha pata nguvu za kutosha kwa ajili ya shambulio jipya kuzipinga nguvu za tabaka zinazotawala, iliundwa Jumuiya ya Wafanya kazi wa Dunia yaani International. Madhumuni yake yalikuwa ni kuwaunganisha pamoja wafanya kazi wote wa Ulaya na Amerika kuwa jeshi moja kubwa. Kwa hivyo haikuweza kuzifuata kwa unyofu kanuni zilizowekwa ndani ya "Maelezo". Ilibidi iwe na mpango ambao hautavizuilia kuingia vyama vya wafanya kazi vya Kiingereza, wafuasi wa Proudhon[8] wa Kifaransa, Kibeljiki, Kitaliana na wa Kispanish na wafuasi wa Lassalle[9] wa Kijerumani. Mpango huu - dibaji ya Kanuni za International - uliandikwa na Marks kwa uhodari mkubwa sana unaosifiwa hata na Bakunin na wanaoamini juu ya kuweko nchi bila ya serikali. Marks alikuwa na matumaini sana ya kufanikiwa mwishowe kwa mawazo yaliyomo ndani ya "Maelezo" akitegemea moja kwa moja juu ya ukuaji wa akili wa tabaka ya wafanya kazi, kama ilivyokuwa lazima utokee kutokana na matendo ya pamoja na mashauriano. Matukio na mageuzo ya mapigano dhidi ya rasilmali, kushindwa hata zaidi kuliko kushinda, ndiko kulikowafunua macho wapiganaji juu ya upungufu wa njia za kuleta nafuu ulimwenguni walizozitegemea kabla, na kuzifanya akili zao ziweze kupokea zaidi fahamu barabara ya hali za kweli za ukombozi wa wafanya kazi. Na Marks alikuwa barabara. Tabaka ya wafanya kazi ya mwaka 1874, wakati wa kuvunjwa kwa International, ilikuwa tofauti kabisa na ile ya mwaka 1864, wakati wa uanzishwaji wake. Mawazo ya Proudhon katika nchi za Kilatini na mawazo ya Lassalle katika Ujerumani yalikuwa yakififia, na hata vyama vya wafanya kazi vya Uingereza vya wakati huo vilivyokuwa ndio nguzo ya wahifadhi wakubwa vilikuwa pole pole vikifika hadi ambapo mwaka 1887 mwenye kiti wa Mkutano wao Mkuu katika Swansea aliweza kusema kwa niaba yao: "Usoshialist wa Kontinenti haututishi tena." Lakini Usoshialist wa Kontinenti mwaka 1887 ulikuwa takriban ni mawazo tu yatangazwayo katika "Maelezo". Basi taarikh ya "Maelezo" kwa daraja maalum ni taarikh ya nyendo za kisasa za wafanya kazi tangu mwaka 1848. Kwa sasa, bila ya shaka, ni yenye kuenea sana kabisa, ni yenye kutolewa katika nchi nyingi sana za dunia kupita maandishi yote ya kisoshialist, ni mpango wa pamoja wa mamilioni mengi ya wafanya kazi wa nchi zote kutoka Siberia hadi California.

Juu ya hivyo, yalipotokeza hatukuweza kuyaita "Maelezo ya Kisoshialist". Katika mwaka 1847 aina mbili za watu ndio waliokuwa wakionekana kama wasoshialist. Upande mmoja palikuwa ni wafuasi wa taratibu za aina mbalimbali za ndotoni, hasa akina Owen katika Uingereza na akina Fourier katika Ufaransa; makundi yote haya mawili yamekwisha pungua na kuwa mafarakano madogo tu yanayofifia pole pole. Kwa upande mwingine, aina nyingi za waganga wanaojidai kutaka kuuletea nafuu ujamaa ambao walitaka kuondosha maafa у a ujamaa kwa njia zao mbalimbali za kufariji na aina zote za kuziba ziba, bila ya kuidhuru hata kidogo rasilmali na faida. Katika hali zote mbili ni watu waliosimama nje ya nyendo za wafanya kazi na waliokuwa wakitaraji msaada hasa kutoka kwa tabaka za "waliosoma". Lakini, sehemu ya wafanya kazi, ambayo ilidai ubadilishwaji mkubwa wa ujamaa, yenye kuamini kwamba haitoshi kufanya thawra ya kisiasa tu, basi ikajiita wakomunist. Ulikuwa bado ukomunist uliobubutika, wenye kusababishwa na hisi ya ndani ya nafsi tu na mara nyingi ni ukomunist kidogo uliokuwa si safi. Hata hivyo ulikuwa ni wenye nguvu za kutosha kubuni taratibu mbili za ukomunist wa ndotoni - katika Ufaransa, ukomunist "wa Ikaria"[10] wa Cabet na katika Ujerumani kulikuwa na ukomunist wa Weitling.[11] Usoshialist katika mwaka 1847 ulileta maana ya mwendo wa kibepari, ukomunist - mwendo wa wafanya kazi. Usoshialist katika Kontinenti kidogo ukiheshimiwa, ambapo kwamba ukomunist ulikuwa ni kinyume cha hayo. Na kama ilivyokuwa sisi tumeshaamini zamani. sana kwamba "ukombozi wa wafanya kazi uwe ni tendo la wafanya kazi wenyewe", tusingaliweza kusita sita juu ya lipi linalofaa tuchukue katika majina hayo mawili. Wala baadaye haijapata kututokelea tulikatae.

“Wafanya kazi wa nchi zote, unganeni!" Sauti chache tu ziliitika tulipotangaza uwito huo ulimwenguni miaka arobaini na mbili iliyopita, karibu na kupambazukia Thawra ya Paris, thawra ya mwanzo ambapo wafanya kazi walijitokeza na madai yao wenyewe. Lakini tarehe 28 Septemba, mwaka 1864, wafanya kazi wa nchi nyingi sana za Ulaya ya Magharibi waliungana katika Jumuiya ya Wafanya kazi wa Dunia у a ukumbusho mtukufu. Kweli, Jumuiya hiyo yenyewe ilidumu kwa muda wa miaka tisa tu, lakini umoja wa milele wa wafanya kazi wa nchi zote ulioundwa nayo bado ungali hai na unaendelea kuwa na nguvu zaidi kuliko zamani, hapana ushuhuda mkubwa zaidi wa hayo kama siku hii ya leo. Kwani leo, niandikapo maneno haya, wafanya kazi wa Ulaya na Amerika wanazipima nguvu zao za kupigana, zilizounganishwa kwa тага уa mwanzo, kama jeshi moja, chini у a bendera moja, kwa ajili ya lengo lao moja la sasa hivi: kiwango cha kufanya kazi saa nane kutwa, kianzishwe kwa kufanywa sheria, kama ilivyotangazwa na Mkutano Mkuu wa International uliofanywa Geneva katika mwaka 1866, na pia na Mkutano Mkuu wa wafanya kazi wa Paris katika mwaka 1889. Na mambo yafanyikanayo leo yatawafunua macho makepitalist na mabwana shamba wa nchi zote kwa ukweli huo kuwa leo wafanya kazi wa nchi zote hakika wameungana.

Laiti kama Marks angalikuwa bado ubavuni pangu kuyaona haya kwa macho yake mwenyewe!

F. Engels

London, tarehe 1 Mai, 1890

________________________

[1] Engels anakusudia Utangulizi wake kwa mchapo wa Kijerumani wa mwaka 1883. (Mteng.)

[2] Tazama maelezo ya uk. 16. (Mteng.) [katika toleo la 1965 katika Swaihili kutoka Idara  ya Maendeleo - Moscow (MIA)]

[3] Maandishi ya asili ya Kijerumani ya Utangulizi wa mchapo wa Kirusi yaliyopotea yameonekana na yamewekwa katika nyumba ya kuhifadhia hati za kitaarikh ya Chuo Kikuu cha Mafunzo ya Marks na Lenin mjini Moscow. (Mteng.)

[4] Tazama maelezo ya uk. 9. (Mteng.) [katika toleo la 1965 katika Swaihili kutoka Idara  ya Maendeleo - Moscow (MIA)]

[5] Tazama maelezo ya uk. 16. (Mteng.) [katika toleo la 1965 katika Swaihili kutoka Idara  ya Maendeleo - Moscow (MIA)]

[6] Tafsiri ya Kispanish ya "Maelezo ya Chama cha Kikomunist" imechapwa katika gazeti El Socialista katika Julai-Agosti, 1886. (Mteng.)

[7] "Maelezo ya Chama cha Kikomunist", yameandikwa na Karl Marks na Frederick Engels. Tafsiri halisi ya Kiingereza yenye kutengenezwa na kuelezewa na Frederick Engels. (Mteng.)

[8] Tazama uk. 66. (Mteng.)  [katika toleo la 1965 katika Swaihili kutoka Idara  ya Maendeleo - Moscow (MIA)]

[9] Lassalle binafsi yake, kwetu sisi, siku zote alijiteta kuwa ni mfuasi wa Marks, na kwa hivyo, alisimama, bila ya shaka kayafuata "Maelezo". Ilikuwa vingine kabisa kuhusu wale wafuasi wake ambao hawakupindukia zaidi ya dai lake la kufanywa shirika za machumo zenye kusaidiwa na mikopo ya kiserikali na ambao waliigawa tabaka nzima ya wafanya kazi katika mapande ya wale wanaopendelea msaada wa kiserikali na wale wanaopendelea kujisaidia wenyewe. (Maelezo yamefanywa na Engels.)

[10] Таz maelezo ya uk. 17. (Mteng.)  [katika toleo la 1965 katika Swaihili kutoka Idara  ya Maendeleo - Moscow (MIA)]

[11] Taz, maelezo ya uk. 18. (Mteng.)   [katika toleo la 1965 katika Swaihili kutoka Idara  ya Maendeleo - Moscow (MIA)]