Maelezo ya chama cha kikomunist

 

UTANGULIZI KWA MCHAPO WA KIPOLISH WA MWAKA 1892

 

F. Engels

 


Tarehe ya kuandika: Katika februari 1892, kwa Friedrich Engels.
Tarehe ya kuchapishwa: Katika 1892.
Toleo hili: Marxists Internet Archive (marxists.org),februari 2013.
Chanzo cha Nakala: Karl Marks na Frederick Engels, Maelezo y Chama cha Kikomunist, Moscow, Idara ya Maendeleo (1965).


 

 

Huo ukweli kwamba pamekuwa pakihitajiwa mchapo mpya wa Kipolish unasababisha ziweko fikira nyingi.

Kabla ya yote, ni jambo linalofaa kuangaliwa kwamba karibuni "Maelezo” yamekuwa ni alama ya kuonyesha usitawi wa uchumi mkubwa katika Kontinenti la Ulaya. Kwa kadiri ya ukubwa wa uchumi ukuavyo katika nchi fulani, ndivyo vivyo hivyo ha ja inavyokua miongoni mwa wafanya kazi wa nchi ile kwa kutaka uongofu juu у a hali yao kama ndio tabaka ya wafanya kazi kuhusiana na tabaka zenye mali; hyendo za kisoshialist zinaenea miongoni mwao na haja ya kuyapata "Maelezo" inazidi. Hivyo basi, si hali ya nyendo za wafanya kazi tu lakini pia kiasi cha usitawi wa uchumi mkubwa kinaweza kupimwa kwa usawa halisi katika kila nchi kwa idadi ya nakala za "Maelezo" zilizotapakanywa kwa lugha ya nchi hiyo.

Vivyo hivyo, mchapo mpya wa Kipolish unaonyesha maendeleo makubwa ya uchumi wa Poland. Na hapana shaka juu ya kwamba maendeleo haya tangu mchapo uliotangulia uliochapwa miaka kumi nyuma yametokea kweli. Ufalme wa Poland, Poland ya Mkutano Mkuu[1], imekuwa sehemu kubwa ya uchumi ya Dola ya Urusi. Ambapo kwamba uchumi mkubwa wa Urusi umetawanyika hapa na pale - sehemu moja kuzunguka Ghuba ya Finland, nyingine iko katika sehemu ya katikati (yaani ya mji wa Moscow na Vladimir), ya tatu imo pwani pwani mwa Bahari Nyeusi na ya Azov, bado nyingine ziko kwingineuchumi wa Poland umekusanyika pamoja katika sehemu ndogo sana na inapata zote mbili faida na hasara ya kukusanyika kama huko. Wenye makarakana washindani wa Urusi walizitambua faida zake walipodai zifanywe hati za ushuru ili kujihifadhi na Poland, ijapokuwa walikuwa na hamu kubwa ya kutaka kuwabadilisha Wapoland wawe Warusi. Hasara - kwa wenye makarakana wa Poland na serikali ya Kirusi - zinaonekana katika utapakaaji wa mbio mbio wa mawazo ya kisoshialist miongoni mwa wafanya kazi wa Kipolish na haja yao ikuayo ya kutaka wapate "Maelezo".

Lakini ukuaji wa haraka wa uchumi wa Kipolish, ukiupita ule wa Urusi, kwa upande wake ni ushahidi mpya wa nguvu zisizokwisha za watu wa Kipolish na dhamana ya ufufuaji tena wa nchi yao. Na kuifufua Poland huru na yenye nguvu, si jambo la Wapoland реке yao, bali ni letu sote. Mashirikiano ya kweli ya kilimwengu ya watu wa Ulaya hayawezekani mpaka isipokuwa kila moja yao wana utawala wao wenyewe nyumbani kwao. Thawra ya mwaka 1848, ambayo chini ya bendera ya wafanya kazi, imekuja kugunduliwa kwamba iliwaachilia wafanya kazi wapiganao kufanya kazi ya mabepari, pia ilizipatia uhuru wake Taliana, Ujerumani na Hungary kwa msaada wa wale wanaotekeleza nia zake - Louis Bonaparte na Bismarck; lakini Poland, ambayo tangu mwaka 1792 imefanya mengi zaidi kwa ajili у a Thawra kuliko nchi zote tatu hizo zikichanganywa pamoja, iliachwa ijimudu wenyewe wakati ilipokuwa ikishindwa katika mwaka 1863 na nguvu kubwa zaidi kwa mara kumi ya Urusi. Watukufu wenye mashamba madogo wa Poland hawakuweza kulinda wala kuukamata tena uhuru wa Poland; leo uhuru huu ndio ni mamoja kabisa kwa mabepari. Juu ya hivyo, unahitajika sana kwa ajili ya mashirikiano mazuri ya nchi za Ulaya. Unaweza kupatikana na tabaka changa tu ya wafanya kazi wa Kipoland na mikononi mwake utathibitika. Kwani wafanya kazi wa nchi zote zilizosalia Ulaya wanauhitajia sana uhuru wa Poland kama wanavyouhitajia wenyewe wafanya kazi wa Kipoland.

F. Engels

London, tarehe 10 Februari, 1892

___________________________________

[1] Poland ya Mkutano Mkuu - ile sehemu ya Poland iliyoingizwa Urusi kwa jina rasmi la Ufalme wa Poland kwa mujibu wa maazimio ya Mkutano mkuu wa Vienna katika 1814-1815. (Mteng.)